USAJILI: Simba yamuwahi mchezaji aliyetajwa Kutua Yanga

0
10
USAJILI: Simba yamuwahi mchezaji aliyetajwa Kutua Yanga sasa kula mwaka mmoja
 Ligi Inaelekea mwishoni kipindi ambacho wachezaji wengi wanaelekea kumaliza Mikataba yao na huenda wakaingia mikataba mipya na Timu zao au wakaamua Kutafuta malisho sehemu nyingine ndani au kubakia nchini.
Yanga na Simba mara kadhaa zimewahi kuwa na Tabia ya Kuchukuliana wachezaji na Ikumbukwe hata wakati wa usajili wa Msimu Huu Simba waliinasa saini ya Haruna Niyonzima kutoka Yanga.
Yanga nao hawakupoa wakamsaini Ibrahim Ajibu kutoka Simba, Sasa mmoja ya wachezaji waliokuwa wakitajwa tajwa kutua Yanga Msimu Ujao wa Ligi ni Said Khamis Ndemla ila kuna AMBAYE  mkataba wake msomaji wa Kwataunit.com unamalizika msimu Huu.
Kuna Taarifa za Uhakika kutoka Simba msomaji wa Kwataunit.com  Kuwa wapo katika mchakato wa Kuhakikisha Ndemla anaongezewa Mkataba wa Mwaka Mmoja kuendelea Kutumikia Simba.
“Kuna wachezaji wetu ambao hatutahitaji kuwapoteza, akiwemo Ndemla hivyo tumeamua kumwongezea mkataba,suala la  Sweden walituahidi hadi msimu ujao kuja kuzungumza,” 
Alieleza Mtoa Taarifa
Chanzo:KwataUnit

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here