Ukiachana na Mkude,wawili kikosi cha 1 hatihati kukosekana dhidi ya Lipuli

0
5
Ukiachana na Mkude,wawili kikosi cha 1 hatihati kukosekana dhidi ya Lipuli. Jumamosi katika uwanja wa Samora Mkoani Iringa kutakuwa na Mchezo kati ya Lipuli Wanapaluhengo kutoka Iringa watakaokuwa wenyeji wa Simba Vinara wa Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara.

Mpaka sasa msomaji wa Kwataunit mchezaji mmoja wa Simba Jonas Mkude ndiye atakayekosekana kutokana na Kuwa na Kadi 3 za Njano kadi ambazo alizipata katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons.
Kuelekea Mchezo huo wa Jumamosi Simba huenda ikawaweka Pembeni Golikipa Aishi Manula na Mshambuliaji wa Kiganda Emmanuel Okwi.
Benchi la Ufundi huenda likawaweka Wachezaji hao benchi kwakuwa wanakadi 2 za Njano na wanajua fika baada ya mchezo wa Lipuli kutakuwa na Dar Darby Simba Vs Yanga na Kama wachezaji hao muhimu wa Kikosi cha kwanza wakipata kadi za Njano basi wataukosa mchezo dhidi ya Yanga.
Chanzo:kwata Unit

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here