Tshishimbi azusha hofu Yanga

0
10
Hawassa, Ethiopia. ‘Hakuna ushindi usiokuwa na kilio’ ndicho kinachoikumba Yanga wakiwa na furaha ya kufuzu kwa hatua ya makundi wamepata pigo la kuumia kwa kiungo wake Pappy Tshishimbi.

Tshishimbi alicheza dakika 67 pekee baada ya kuhisi maumivu makali katika mguu wake katika mchezo wa jana dhidi ya Welayta Dicha na kutolewa nafasi yake kuingia Emmanuel Martin.
Leo wakati Yanga ikiondoka Hawassa meneja wa timu hiyo Hafidh Saleh alisema bado madaktari wanafuatilia kwa karibu afya ya kiungo wao huyo.
Saleh alisema maumivu aliyoyapata Tshishimbi sio makubwa, lakini wanataka kuchukua tahadhari kuhakikisha anakuwa sawa haraka kabla ya mchezo ujao, lakini wachezaji wengine wote wako sawa.
“Kila mchezaji yuko sawa isipokuwa Tshishimbi ambaye jana alipata maumivu, lakini madaktari wetu wanafanya juhudi kubwa kufuatilia afya yake kwa ukaribu na hakuumia sana ni maumivu ya kawaida,”alisema Saleh.
Chanzo: Mwananchi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here