Tetesi za soka Ulaya 11.04.2018: Timu zinajipanga kwa msimu ujao

0
8

Anthony Martial hataki kuendelea kuichezea Manchester United

Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 22, amekataa mkataba wa miaka mitano na anataka kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu.

Martial angetaka kubakia Manchester United lakini meneja Jose Mourinho anaweza kumuona kama mchezaji mbadala huku Juventus, Paris St-Germain na Atletico Madrid wote wakimtaka mshambuliaji huyo wa Ufaransa (Independent)
Tottenham na Inter Milan pia wako makini na Martial ikiwa ataambiwa naweza kuondoka Old Trafford. (Telegraph)

Antoine Griezmann nchezaji wa Atletico Madrid Mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 25, alipendekezewa kujiunga na timu za Real Madridpamoja na Manchester City mwezi Januari na wakala wa Mino Raiola. (Sports Illustrated)
Atletico Madrid wako tayari kutoa Euro 300,000 za ziada kusiani mkataba na Antoine Griezmann wiki moja kumzuwia mshambuliaji huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 27- kuihama klabu mwishoni mwa msimu huu. (Mirror) e umri wa miaka 18. (Sun)
Rais wa Roma James Pallotta amepinga madai ya kuondoka kwa mlinda lango Alisson katika klabu hiyo msimu huu, huku Liverpool wakimtaka mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 (Football Italia)
Mtendaji Mkuu wa Juventus Giuseppe Marotta anasema anataka mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, mwenye umri wa miaka 24, kuamua ikiwa anataka kujiunga na klabu hiyo katika muda wa siku 10 zijazo au la , huku mahasimu wao Real Madrid na Bayern Munich wakiashiria kuwa wanamtaka. (Tuttosport – in Italian)

Mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool na Ujerumani Emre Can Paris St-Germain wanakaribia kufikia uamuzi wao wa mwisho juu ya nani atakayechukua nafasi ya Meneja Unai Emery msimu ujao baada ya kufanya mazungumzo na wawakilishi wa meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel. Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo. (Guardian)

(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
Washindi wa ligi ya Italia pia wanaangalia uwezekano wa kumchukua Mousa Dembele, Mchezaji wa safu ya kati wa 30 timu za Tottenham na Ubegiji . (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 28, haondoki Real Madrid msimu huu, licha ya kuwa nje katika mechi muhimu kadhaa hivi karibuni ,anasema wakala wake. (ESPN)
Mlinda lango wa Aston Villa Sam Johnstone mwenye umri wa miaka 25 , ambaye ana deni la Manchester United, amesema kuwa ataondoka Old Trafford na anaweza kwenda Villa Park. (Guardian)

Mlinzi wa timu ya England ya vijana walio chini ya umri wa miaka 19 Ben Wilmot Norwich inaweza kulazimika kumuuza mchezaji wake wa safu ya kati James Maddison mweney umri wa miaka 21- msimu huu, huku Liverpool na Tottenham wakiashiria kumtaka. (Mirror)
Valencia wanataka kusaini mkataba wa kudumu na mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Mbrazil Andreas Pereira, mwenye umri wa miaka 22. (AS – in Spanish)
Watford hawana tena haja na mlinzi wa timu ya England ya vijana walio chini ya umri wa miaka 19 Ben Wilmot, huku Arsenal na Tottenham wakiwa bado wanashindania kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18. (Sun)
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); Mshambuliaji Forward Reiss Nelson, mwenye umri wa miaka 8, anatumai kusaini mkataba na Arsenal mara baada ya kuanza mchezo wake wa kwanza katika Ligi kuu ya Primia kufuatia ushindi wake wa Jumapili dhidi ya Southampton. (Sky Sports)
Mwandishi wa taarifa za soka nchini Italia James Horncastle anasema Meneja Antonio Conte atahangaika kupata kazi ya Meneja msimu huu ikiwa ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu. (BBC Radio 5 live)
chanzo-bbc swahili
by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here