Tetesi za Soka Barani Ulaya leo Alhamisi 19/04/2018

0
3
Patrick Vieira
Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal na mkufunzi wa klabu ya New York City nchini Marekani Patrick Vieira ni miongoni mwa wakufunzi walioorodheshwa kumrithi mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger atakapostaafu. (Mail)
Klabu ya Tottenham inataka kumnunua winga wa klabu ya Leicester 21 Demarai Gray. Tottenham ilitaka kumsajili Gray msimu wa dirisha la uhamisho ulioisha lakini The Foxes walikataa maombi yanayowasilishwa ya nahodha huyo wa timu ya wachezaji wasiozidi miaka 21 nchini Uingereza (ESPN)
Mkufunzi wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino anamtaka beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa, 25
Mkufunzi wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino anamtaka beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa, 25, lakini anaweza kukabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Chelsea kumpata raia huyo wa Ufaransa. (Mirror)
Lyon na Juventus wanataka kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 22. (Sun
Anthony Martial
Arsenal pia walikuwa wanamnyatia lakini Wenger ameamua kuimarisha safu nyengine za kikosi chake mwisho wa msimu huu. (Evening Standard)
Mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri ndio chaguo la kwanza la Chelsea kuchukua mahala pake Antonio Conte.
Wachezaji kadhaa wanaolengwa na Chelsea mwisho wa msimu huu hawataandikisha mikataba hadi watakapobaini ni nani atakayekuwa mkufunzi wa klabu hiyo. (Mail)
Mmiliki wa Chelsea Roman Abrahamovic
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ametakiwa kumsajili kinda anayeinukia badala ya wachezaji maarufu.. (Telegraph)
Hatahivyo usimamizi wa klabu hiyo unatofautiana kuhusu ni nani atakayemrithi raia huyo wa Ufaransa huku kocha wa zamani wa Barcelona Louis Enrique pia akilengwa. (Telegraph)
Liverpool inataka kumsaini kiungo wa kati wa Portugal Ruben Neves, 21, kutoka klabu mpya iliopandishwa daraja Wolverhampton Wanderers. (Talksport)
Crystal Palace itamuuza mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 27, mwisho wa msimu huu. (Mail)
Klabu ya Wolves iko tayari kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere, 26, ambaye huenda akaondoka Arsenal kama mchezaji huru mwisho wa msimu huu na tayari klabu ya Everton imewasilisha ombi kubwa. (mirror)
Tottenham itaongeza kandarasi ya mshambuliaji Erik Lamela kwa mwaka mmoja hatua itakayomuweka mchezaji huyo wa Argentina katika klabu hiyo hadi 2020. (Independent)
Source:BBC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here