TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMATANO 18/04/2018

0
1
Mourinho
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Fred kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk ili kuchukua mahala pake Paul Pogba. Manchester City pia inamnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.. (Mirror)
Real Madrid inataka kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Pogba lakini rais Florentino Perez anasema kuwa hawezi kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hadi pale atakapopunguza mshahara wake na kuonyesha mchezo mzuri wakati wa kombe la dunia nchini Urusi. (Express)
Manchester City Inalenga kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kyllian Mbappe, 19, na kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara katika uwanja wa Etihad mwisho wa msimu huu (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Norwich City na Uingereza James Maddison, 21, anasakwa na vilabu kadhaa katika ligi ya Premia ikiwemo Tottenham, Arsenal, Everton na Manchester City. (Telegraph)
Borussia Dortmund inataka kumsajili Michy Batshuayi, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Chelsea, kwa kandarasi ya kudumu mwisho wa msimu huu.Chelsea inataka zaidi ya £50m ili kumuuza mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24. (Evening Standard)
Chelsea inataka kumsajili kiungo wa kati wa Nice Jean Michael Seri kwa dau la £35m, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Ivory Coast anatarajiwa kusubiri na kuona ni nani mkufunzi wa Blues msimu ujao. (Mirror)
Beki wa kushoto Luke Shaw hajaamua kuhusu hatma yake katika klabu ya Manchester United . Mchzaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ataamua mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuwa na uusiano mbaya na Mourinho.. (ESPN)
Barcelona imetenga kitita cha £60m ili kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 22, huku mchezaji wa Fulham Ryan Sessegnon, 17,pia akiripopotiwa kusakwa na klabu hiyo.. (Mail)
Liverpool na Tottenham walikuwa miongoni mwa klabu nyingi za ligi ya Uingereza kutuma maskauti wake kumtazama winga wa Benfica na Serbia Andrija Zivkovic siku ya Jumapili katika mechi na Porto. (Sun)
Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino anaamini dirisha fupi la mwisho wa msimu litatoa fursa kwa Tottenham kuanza vizuri katika ligi ya Uingereza. (ESPN)
Huddersfield itampatia meneja wake David Wagner kandarasi mpya ya miaka miwili na mshara mpya Mkufunzi huyo alikuwa amehusishwa na uhamisho wa kurudi klabu ya Borussia Dortmund. (Sun via Huddersfield Examiner)
Chanzo: BBC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here