Tetesi Za Soka Barani Ulaya leo Juma Pili

0
5
Arsene Wenger alikuwa anafahamu wiki nne kabla ya kutangaza kuwa ataondoka katika klabu ya Arsenal mwishoni mwa msimu huu (Mail)
Arsenal wana nafasi ya kumteua meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique kuwa mbadala wa Arsene Wenger baada ya kuonekana kuwa klabu ya Chelsea imetulia kuhusu suala la kumchukua kocha huyo, taarifa zinasema Chelsea wanawafuatilia kwa ukaribu Meneja wa Juvetus Max Allegri na wa Napoli Maurizio Sarri kuja kuchukua nafasi ya Antonio Conte. (Times)
Washika mitutu wa London Arsenal wanaweza mchukua meneja wa Nice ya Ufaransa Lucien Favre, 60, (Bild via The Sun)
Meneja wa Paris St-Germain Unai Emery anaamini Arsene Wenger atakuja kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ya PSG Siku za usoni (Goal) Licha ya , PSG wao kutaka kumpata Wenger’s cheo cha urais wa timu hiyo (Mirror)
Mshambuliaji wa Manchester United Alexis Sanchez amesema hakuweza kuandika chochote kwenye mitandao ya kijamii khusu kocha wake zamani Arsene Wenger bali alimtumia ujumbe moja kwa moja, Sanchez aliongeza kwa kusema kuwa kocha huyo ni mtaalamu wa mpira na anamshukuru.(Sunday Expres)
Meneja wa Man United Jose Mourinho hatomzuia mshambuliaji Anthony Martial kuondoka kama mchezaji huyo atataka kuondoka katika timu hiyo (Times)
Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta mwenye miaka 33 amesema atatoa msimamo wa muelekeo wake wiki hii (Sunday)
Kiungo wa Napoli ya ya Italia Jorginho ameonyesha nia ya kutaka kujiunga na Manchester City kuliko wapinzania wao Man United ambao wanahitaji saini ya fundi huyo wa dimba .(Sun)
Man United wanaangalia uwezekano wa kumsajili mlinzi wa Sevilla Clement Lenglet lakini watakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona ambao pia wanamtaka mchezaji huyo(Sun)
Meneja wa Newcastle Rafa Benitez klabu yake inanafasi ya kumbakisha winga Kennedy ambae huyo klabuni hapo kwa mkopo akitokea Chelsea (Mial on Sunday)
Meneja wa Swansea Carlos Carvalhal amemuelezea meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuwa ni mungu wa mpira wa miguu(Manchester Everning News)
Beki wa Everton Michael Keane anaimani mchezaji mwenzake wa zamani wa Burnley Joey Barton,atafanikiwa katika jukumu la ukocha akiwa na klabu ya Fleewood( Liverpool Echo)
Source: bbc

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here