TCRA Yatoa Hukumu kwa Times Fm Kisa Diamond. Clouds Nayo Yapewa Onyo Kali

0
6

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),imetoa hukumu kwa vituo viwili vya radio vya Times FM na Clouds FM kwa makosa ya ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2018.Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam imesema kuwa Radio ya Times FM walitangaza mahojiano na mwanamziki Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinum.Imeelezwa kwenye mahojiano hayo mwanamuziki huyo alitamka maneno yasiyofaa kimaudhui akimshambulia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza.
“Times FM wamepewa onyo na kutakiwa kumuomba radhi Naibu Waziri Shonza na jamii kwa ukiukwaji huo wa maadili ya utangazaji,”imesema sehemu ya taarifa hiyo.Kuhusu Radio ya Clouds FM ni kwamba imepewa onyo kwa kutozingatia mizania ya utoaji wa habari uliohusu pande mbili ya mwanamuziki Ibrahim Musa a.k.a Roma mkatoliki na Naibu Waziri Shonza.
Chanzo: Udaku Special 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here