Simba na Yanga zagombaniana uwanja wa kambi moro

0
3

Vilabu vya Simba na Yanga zagombania uwanja wa chuo cha biblia Morogoro kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wao wa watani utakaochezwa April 29 uwanja wa Taifa Dar.

Habari kutoka morogoro zinasema Simba na Yanga wote wameandika barua ya kuomba kukitumia kiwanja hicho kama maandalizi ya mchezo huo.

Simba na Yanga watacheza michezo ya Vpl  mwishoni mwa wiki hii kabla ya kucheza mchezo huo. Simba watacheza dhidi ya Lipuli Fc jumamosi ya April 21 mkoani Iringa huku Yanga wakiwa wageni wa Mbeya City April 22.

Pia viingilio vya mchezo wa Simba na Yanga  vimetangazwa mzunguko ni shilingi 7000 tu, VIP B ni 20,000 huku VIP A ni 30,000

Source:@yossima Sitta Jr.
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here