Simba mteremko kwa mbeya city

0
4

Kikosi cha Simba SC Alhamis hii kitakuwa na kibarua dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Simba itakuwa inaingia kucheza mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi dhidi ya Njombe Mji na Mtibwa Sugar katika michezo iliyopita.

Kuelekea mechi hiyo, wapinzani wao Mbeya City watawakosa wachezaji wao wawili, Hassan Mwasapili na John Kabanda.

Kabanda ataukosa mchezo kufuatia kuwa majeruhi huku Mwasapili akitumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano.

Kukosekana kwa wachezaji kunaweza kukaipa mteremko Simba ambayo pia iliwakosa wachezaji wake James Kotei, Erasto Nyoni na Juuko Murushid kwenye mchezo dhidi ya mtibwa jana waliokuwa wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano pia.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here