Simba fiti kuwakabili mtibwa kesho

0
8
Na George Mganga 
Kikosi cha Simba kinafanya mazoezi ya mwisho mjini Morogoro leo, tayari kwa mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa mjini Morogoro kesho Jumatatu.
Simba na Mtibwa zitakuwa zinaingia Jamhuri zikiwa na kumbukumbu ya kupata matokeo kwenye mechi zilizopita, ambapo Simba iliiadhibu Njombe Mji kwa mabao 2-0 huku Mtibwa ikiilaza vikali Singida United 3-0, michezo yote ikipigwa ugenini.
Simba itakuwa kibaruani bila wachezaji wake muhimu watatu ambao wanatumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano.
Beki Juuko Murushid, Erasto Nyoni na Kiungo James Kotei hawataitumikia timu yao kesho sababu ya kuwa na idadi ya hiyo ya kadi za njano, hivyo watalazimika kuisubiri Tanzania Prisons kwenye unaofuata baada ya Mtibwa Sugar.
Licha ya kukosekana wachezaji hao, Kiungo Jonas Mkude anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kufuatia kupona majeraha yake ya kifundo cha mguu aliyoyapata wiki moja iliyopita wakati timu ikijiandaa na mchezo dhidi ya Njombe Mji.
Mkude aliumia kifundo hicho baada ya kukwaana miguu na kiungo mwenzake, Mzamiru Yassin kwenye Uwanja wa Boko Vetarani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here