Simba Afungwa Speed Governor na Lipuli… Ashindwa Kuunguruma Samora.

0
6
KIkosi Cha Simba

Lipuli, a.k.a Ngome, Waite tena “Vana va Paluhengo” wamegeuka kuwa speed governor, au Waite wamegeuka kuwa “kizibiti mwendo” kwa klabu ya Simba katika harakati zake za kuusaka Ubingwa wa VPL Tanzania Bara.
Lipuli wamegoma kuwazawadia Simba alama tatu muhimu wanazozihitaji ili kuendelea kumtambia Mtani wake wa Jadi Yanga na kuendelea kukaa kileleni mwa ligi.

Simba wamepata alama moja kwa taabu sana baada ya kuilazimisha Lipuli sare ya 1-1 katika mchezo uliofanyika Leo jumamosi katika uwanja wa Samora mjini Iringa.

Shukrani za pekee zimuendee Mavugo, “the super sub” aliyeipatia Simba goli hilo la kusawazisha , vinginevyo Simba walikuwa wanatoka uwanjani hapo bila ya alama yeyote.

Katika mchezo huo Mwandishi wetu aliyekuwa uwanjani anaripoti kwamba: Simba walikuwa wamebanwa kwelikweli na Lipuli, Lipuli walimiliki Mpira kwa kiasi kikubwa uwanjani.

Na: sabby@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here