Siku za Conte chelsea zinahesabika

0
9Kufuatia Chelsea kupata matokeo ya kusuasua msimu huu katika Ligi Kuu England, Kocha wa kikosi hicho, Antonio Conte anaweza akafungashiwa virago kabla ya msimu kumalizika.

Taarifa kwa mujibu wa Daily mail zinaeleza kuwa sare ya bao 1-1 aliyoipata kwenye mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya West Ham United inaweza ikawa imechangia kwa kiasi kikubwa Conte kutosalia Darajani.

Chelsea mpaka sasa ipo kwenye nafasi ya msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 57 ikiwa imecheza michezo 32.

Hapo awali taarifa ziliripoti kuwa Conte engeweza kusalia mpaka mwisho wa msimu, lakini kadri siku zinavyokwenda kumeonekana kuwa na mabadiliko kutokana na timu yake kupata matokeo ambayo hayaridhishi kiu ya mashabiki.

Source: Saleh Jembe

Na: Agape Patrick

Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here