Ronaldo afananishwa na mvinyo

0
8
Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri amemfananisha Cristiano Ronaldo na kinywaji cha mvinyo akisema kuwa kadiri umri unavyokwenda ndio anazidi kuwa mkali zaidi. Allegri alimkubali Ronaldo baada ya kuiongoza Real Madrid kuirarua Juventus 3-0 mbele ya mashabiki wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wiki iliyopita.
“Unajua Ronaldo yaani ni sawa na mvinyo kadiri muda unavyokwenda ndio anazidi kuwa bora,” alisema Allegri baada ya mchezo huo, ambao Ronaldo aliacha mashabiki wa soka mdomo wazi baada ya kufunga bao maridadi la ‘tik tak’. Allegri alisema kuwa Ronaldo amekuwa straika bora wa dunia kwa miaka miwili sasa.
 Alisema kuwa pamoja na fowadi huyo kuwa na umri wa miaka 33 lakini bado ana kiwango cha kutisha. Nyota ya Ronaldo bado ipo juu Real Madrid wakati wenzake waliounda kombinesheni ya BBC yaani Gareth Bale na Karim Benzema wakiwa wamechuja siku za karibuni. 
Katika miaka ya nyuma, Ronaldo alikuwa anasifika kwa mbio na chenga lakini kutokana na umri kumtupa mkono siku hizi anahakikisha anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kila mara.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here