Raisi wa Sporting Cp awafungia wachezaji 19 wa kikosi cha kwanza.

0
4

Boss ni boss tu, hicho ndicho unachoweza kusema baada ya wachezaji 19 wa kikosi cha kwanza cha Sporting Cp kusimamishwa kuitumikia timu hiyo baada ya kujaribu kumpinga raisi wa timu hiyo.

Chanzo cha sakata hili ni Athletico Madrid, baada ya Athletico Madrid kuwafunga Sporting Cp mabao 2 kwa 0 hali ambayo iliamsha hadira kwa raisi wa Sporting Bruno de Carvalho na kuamua kuwashambulia wachezaji wake.

Kupitia mtandao wa FaceBook raisi huyo alioneshwa kukerwa kwa kile alichosema kutojituma kwa wachezaji wake na kusema hawajitolei kwa ajili ya timu na ndio maana wanafungwa kirahisi.

Raisi huyo amesema kwamba aina ya timu anayotaka kuwa nayo ni timu ambayo wako 11 uwanjani lakini wawe wanacheza kama wako 22 hali ambayo wachezaji wa Sporting CP hawaioneshi na hawakabi wala kufunga.

Baada ya ujumbe huo wachezaji 18 wa Sporting Cp waliamua kuutuma mitandaoni na kuonesha kutoridhishwa na kile alichofanya raisi wao na hapo ndipo raisi aliamua kuonesha nguvu yake ya uongozi.

Wachezaji 19 ikiwemo nyota Rui Patricio, William Carvalho, Fabio Coentrao, Bruno Fernandes, Gelson Martins, Bryan Ruiz, Sebastian Coates walisimamishwa, na kupitia tena ukurasa wa facebook raisi huyo amesema hatua zaidi zitakuchukuliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here