Pointi 55, mabao 55 yaipa Simba SC usukani wa ligi kuu bara

0
16

Baada ya ushindi wa jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya Mbeya City, vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC hivi sasa imefikisha jumla ya mabao 55.

Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi baada ya kupata goli moja hii anakuwa amefikisha jumla ya mabao 18 na kuongoza kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu nafasi ya pili ikichukuliwa na swahiba wake ndani ya klabu, John Bocco ambaye ana 13 huku ya tatu ikienda kwa Obrey Chirwa aliyefikisha 12 mpaka sasa.
Klabu ya Simba inaongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 55 wakati nafasi ya pili ikiwa chini ya hasimu wake Yanga SC wenye alama 47.
Chanzo: Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here