Paul Bukaba mchezaji bora dhidi ya Mtibwa Sugar

0
14

Klabu ya Simba yamtangaza, Paul Bukaba kuwa mchezaji bora wa mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliyopigwa hapo jana kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro na kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0.

Mchezaji bora wa mechi ndani ya klabu ya Simba hupatikana mara baada ya kupatikana kwa kura zilizopigwa na mashabiki kupitia kurasa mbali mbali za kijamii.
Bukaba amekuwa mchezaji bora wa mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuonesha mchango mkubwa hapo jana.
Kwa mujibu wa kura zilizopigwa na mashabiki kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo, Bukaba alishinda tuzo hiyo baada ya kuonesha mchango mzuri kwenye mchezo huo wa jana.
Simba SC sasa imezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 52  wakati watani wao wajadi Yanga SC wakiwa na alama 46.
by richard@spoti.co.tz
Chanzo: Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here