PANCHA: Ngoma aumia tena mazoezini jioni

0
9

Mshambuliji wa timu ya Yanga, Donald Ngoma ameumia tena mazoezini na hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza kesho na Wolaita Dicha katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika.

Ngoma alisafiri na wachezaji wenzake kuelekea mkoani Singida katika mchezo wa robo fainali ya kombe la FA waliotolewa na Singida United, Aprili mosi baada ya kupona majeraha yake.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa amesema wamemuengua Ngoma katika mchezo huo kutokana na kupata tena maumivu hivyo wachezaji wengine wataziba nafasi yake.

“Ngoma ameumia tena na hatokuwa sehemu ya mchezo wa kesho mpaka atakapokuwa fiti kabisa,” alisema Nsajigwa.

Ngoma amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na maumivu ya goti ambapo alicheza mechi chache za mzunguko wa kwanza wa ligi wakati wa pili hajagusa hata moja.

Mbali na Ngoma wachezaji wengine wakatakao kosa mchezo huo ni pamoja na Amiss Tambwe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu, Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Said Makapu na Obrey Chirwa ambao wanatumikia adhabu ya kadi.

Source:Yanga SC
Na: Agape Patrick
Email:agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here