Okwiiiiii aizamisha Mtibwa

0
1

Morogoro. Mshambuliaji Emmanuel Okwi amefunga bao lake 17 msimu huu akiiongoza Simba kuichapa Mtibwa Sugar 1-0 katika mchezo Ligi Kuu uliomalizika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Ushindi huo unaifanya Simba kuongoza ligi kwa pointi 52 na kuiacha Yanga iliyokuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi sita hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Wakati Simba ikijikita kileleni naye mshambuliaji Okwi amefunga bao lake la pili nje ya Dar es Salaam msimu huu na kumfanya kufikisha mabao 17 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kunyakuwa tuzo ya mfungaji bora msimu huu.
Okwi alifunga bao lake katika dakika 23, akiunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na John Bocco aliyepokea krosi ya Kichuya na kutegeneza nafasi hiyo iliyomkuta Mganda huyo aliyeumbukiza mpira wavuni na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Simba waliofurika uwanjani hapo.
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na dakika ya pili, kipa wa Mtibwa, Tinoco alifanya mzaha mpira unachukuliwa na Bocco ila kabla hajafanya lolote anafanikiwa kuutoa na kuwa wa kurusha, katika tukio hilo kipa huyo aliumia na madaktari kuanza kumtiabia
Simba iliendelea kulishambulia lango la Mtibwa na dakika 4, Kapombe alipiga shuti nje ya 18, linatoka nje na dakika 12, krosi Kichuya inapanguliwa na Tinoco.
Dakika 23, krosi ya Kichuya anatua katika kichwa cha Bocco ambaye anampa pasi ya kichwa Okwi anafunga goli la kwanza kwa Simba, baada ya bao hilo Mtibwa iliamka na dakika 26, wanapata faulo inapigwa inapaa juu ya goli la Simba
Dakika ya 30, Mtibwa wanapata kona inapigwa na Kihimbwa beki wa kati Dickson anamalizia kwa kichwa inapaa juu ya goli la Simba, kasi hiyo ya mchezo inawalazimisha wachezaji wa kiungo Dilunga wa Mtibwa na Mkude wa Simba wanapewa kadi za njano baada ya kuacha mpira na kuanza kuzozana na kufanya timu hizo kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-0.
 Kipindi cha pili Simba ilirudi kwa kucheza kwa kujilinda zaidi na kuwaacha Mtibwa Sugar kutawala mchezo huo, lakini washambuliaji wake walikosa umakini katika kumalizia nafasi walizozipata.
Mtibwa iliwatoa Stamili Mbonde, Aidan, Hassan Dilunga na kuwaingiza Hussein Javu, Haruna Chanongo na Semtawa wakati Simba iliwapumzisha Mzamiru Yassin na kuingia Salum Mbonde , pia alitoka Gyan na kuingia Niyonzima
Mabadiliko hayo hayakuwa na faida kubwa kwa timu zote ziliendelea kutegeneza nafasi, lakini walishindwa kuzitumia na kufanya machezo huo kumalizika kwa Simba kushinda kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Jamhuri baada ya misimu mitatu.
PLASTA YAFUNGA NYAVU
Katika hali isiyotarajia mwamuzi Abubakar Mturo alizimika kutumia plasta kufunga nyavu za uwanjani kabla ya  kuanza kwa mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Simba.
Katika goli alilosimama kipa Aish Manula nyavu zilikuwa zimechanika na alipoona mwamuzi wa mchezo huo,   akaamua  kuzifunga ili kuepusha kusitokee hitalafu  katika mchezo huo unaoonekana kuwa mgumu,  Simba ikiwa inasaka  kuendelea kukaa kileleni.
Zoezi la kufunga nyavu hizo likiendelea kipa wa Simba, Manula alikuwa bega kwa bega kuhakikisha anakula salama  katika lango lake.
Msimamo Ligi Kuu  Bara 2017/2018
                          P W     D       L        F       A       PTS
1. Simba        22         15     7       0       52     11     52
2. Yanga         21        13     7       1       38     11     46
3. Azam         23         12     9       2       24     10     45
4. Prisons       23        9       10     4       22     15     37
5. Singida     23          9       9       5       21     21     36
6.Mtibwa     22          7       9       6       18     16     30
7. Lipuli         23         6       10     7       16     17     28
8.Mbeya       23         5       11     7       20     25     26
9. Ruvu           23        6       8       9       20     29     26
10. Stand        23       6       7       10     15     26     25
11.Mwadui    23       4       11     8       24     30     23
12.Ndanda    23        4       11     8       16     22     23
13.Kagera      23        4       10     9       14     23     23
14.Mbao        23       4       8       11     19     30     20
15.Njombe     23       3       9       11     13     31     18
16.Majimaji    23      2       10     11     18     32     16
Chanzo: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here