NUSU FAINALI ZA AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUCHEZWA APRILI 20 NA 21 SHINYANGA NA SINGIDA

0
2

MECHI za Nusu Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kuchezwa Aprili 20 na 21, mwaka huu.
Nusu Fainali ya Kwanza itachezwa Ijumaa ya Aprili 20, 2018 ikiwakutanisha Stand United ya Shinyanga watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kuanzia Saa 10:00 jioni.
Nusu Fainali ya pili baina ya Singida United ya Singida watakaowakaribisha JKT Tanzania ya Dar es Salaam itachezwa Uwanja wa Namfua Jumamosi ya Aprili 21 kiuanzia Saa 10:00 jioni pia na Fainali itachezwa Mei 31.
by richard@sporti.co.tz
Chanzo: Shutikali

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here