Nisingekua hapa bila ya Kanumba- Rose Ndauka

0
1

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Rose Ndauka amefunguka na kudai bila ya mafundisho na ushauri aliyopewa hapo awali na marehemu Steven Kanumba, muda huu watanzania na watu wengine wasingeweza kumtambua kama mmoja wa wasanii wazuri.

Ndauka ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo na kusema Tanzania na dunia kiujumla itaendelea kumkumbuka marehemu Kanumba kutokana na ubora na uzuri wa kazi zake alizokuwa akifanya.
Ushauri wako bado naufatisha. Waswahili husema rafiki wa kweli sio yule atakae kupa samaki ukiwa na njaa bali ni yule atakae kufundisha kuvua samaki ili kesho uweze kukidhi mahitaji yako hata ukiwa mwenyewe pia uweze kuambukiza ujuzi huo wengine. Ulinifunza vyema, nisingekua hapa umekua sababu kubwa ya hapa nilipo. Tutakukumbuka Daima na milele… ‘Rest In Peace Teacher“, amesema Ndauka.
Rose Ndauka ametoa hisia zake hizo kwa jamii ikiwa leo siku ya kumbukumbu ya kifo cha marehemu Steven Kanumba. Aliyekuwa nguli wa bongo ‘movies’ ndani na nchi na nje ya mipaka ya Tanzania.
Chanzo: EATV

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here