Neymar atarajia kurudi katika Kombe la Dunia baada ya kupoa mguu aliovunjika

0
8

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar anatarajiwa kuwa katika afya nzuri kuweza kushiriki katika Kombe la Dunia msimu huu wa joto na anasema atarudi katika mazoezi Mei 17 baada ya kuwa nje kufuatia kuvunjika mguu.Mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa Paris St-Germain alihitaji kufanyiwa upasuaji mfupa baada ya kujeruhiwa katika mechi ya ligimnamo Februari 25.Brazil inacheza mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Switzerland Juni 17, mwezi mmoja baada ya muda anaotarajiwa kurudi uwanjani.
“Natarajia kurudi nikiwa fiti kabisa,” amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.Neymar alikuwa mchezaji mwenye gharama ya juu wa soka alipojiunga na PSG kutoka Barcelona Agosti mwaka jana, na amefanikiwa kufungua magoli 25 huku akiwa amesaidia kufanikisha mara 16 kufunga kwa timu hiyo ya Ufaransa msimu huu.“Nafanyiwa ukaguzi wa mwisho Mei 17 na baada ya hapo nitaweza kucheza,” ameambia mkutano wa waandishi habari mjini Sao Paulo, ambako amekuwa akipokea matibabu.”Ninafanyiwa ukaguzi kila siku, na kuanzia nitakapo anza kufanya mazoezi nitatia bidiii zaidi ya nilivyokuwa nikijitahidi kwasababu hii ni ndoto inayokuja. Ni Kombe la Dunia.Nimesubiri miaka minne kwa nafasi hii, ipo karibu.”
Neymar aliichezea Brazil iliyoshinda Kombe la Dunia mara tano, katika fainali za mwaka 2014 nyumbani lakini alikosa kushiriki mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani kutokana na jeraha na timu hiyo ilifungwa 7-1.
Brazil itaelekea Urusi pamoja na Ujerumani.Baada ya goli la ufunguzi dhidi ya Switzerland katika kundi E, watakabiliana na Costa Rica Juni 22 na baadaye Serbia siku tano baadaye.Neymar, aliyejiunga na PSG kwa kitita cha Pauni milioni 200, sanasema ana shauku kusukuma tobwe baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi mitatu sasa. “Ni wazi kuwa bado kuna wasiwasi na mwenyewe saa nyingine huhisi,” amesema. “lakini hilo ni jambo la kawaida kwa mtu aliyefanyiwa upasuaji kwa mara ya kwanza tangu nianze kucheza mpira wa kulipwa. Ni vigumu kwangu mimi kutocheza na pia kufanya mazoezi.
“Ni lazima nijitahidi zaidi lakini nitakuwana muda wa kutosha kuwasili nikiwa katika afya nzuri katika Kombe la Dunia, kujitayarisha.Nilihisi vibaya nilipojeruhiwa, lakini nimepumzika vizuri, hayondio manufaa, ni lazima tutazame manufaa mazuri ya hali zilizopo.”

Posted by Lebab
Source: Bbc swahili

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here