Mvua kubwa inayonyesha Dar es Salaam Tanzania hivi sasa imetatiza huduma za usafiri kwa mabasi ya mwendokasi na hata magari binafsi

0
3
Mvua kubwa inayonyesha Dar es Salaam Tanzania hivi sasa imetatiza huduma za usafiri kwa mabasi ya mwendokasi na hata magari binafsi.
mathalani, usafiri wa mabasi ya mwendo kasi umesitishwa kutokana na mafuriko eneo la Jangwani.
Muandishi wa BBC Mjini Dar es Salaam anaeleza kuwa kila mvua kubwa inaponyesha huduma za mabasi hayo husitishwa kutokana na sababu kadhaa.
Mojawapo ya sababu ni kufurika maji kwa njia ambazo mabasi hayo yanapitia na pia kufurika maji kwenye kituo hicho kikuu ambapo mara ya mwisho mabasi kadhaa yaliharibika sababu ya kujaa maji.
Sababu nyingine ni kukatika kwa umeme kwenye vituo vyake wakati wa mvua – hivyobasi kusababisha kukwama kwa mfumo wake wa ukataji tiketi.
Mvua inaponyesha jijini hapa huwa kuwa na usumbufu wa hali ya juu sana kwa wakazi wake, hii hutokana na ukweli kwamba maji hutuama sana katika njia, bado kuna wakaazi wengi wa mabondeni, miundombinu nayo ni tatizo jingine. miundombinu kuharibika wakati mwingine kunatokana na wakaazi wa jiji hili kutokuwa na utamaduni mzuri wa kutunza miundombinu hiyo. mara nyingi utakutana na uchafu mwingi kama mifuko ya plastiki, taka zitokanazo na matumizi nyumbani zikiwa zimetupwa katika mifereji ya kusafirishia maji haya wakati kama huu na hivyo kupelekea maji kukosa njia na kutuama kila mahali.
Chanzo: bbc
sabby@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here