Mtibwa Sugar kuivurugia Simba Leo Bila Okwi

0
9
Harakati wa kusaka ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2017/18, zinaendelea leo kwa mchezo mmoja utakaoshuhudia Wekundu Wa Msimbazi Simba wakipapatuana na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.
Simba ambao ndiyo vinara wa ligi hiyo kwa sasa, watalazimika kusaka ushindi ili kujisafishia njia ya kutwaa ubingwa wa Tanzania bara, ambao pia unawaniwa na mahasimu wao katika soka la bongo Young Africans.
Hata hivyo Simba wataingia uwanjani hii leo huku wakiwakosa wachezaji wao watatu kutokana na kuwa na kadi tatu za njano, ambao ni Erasto Nyoni, Juuko Murshid na James Kotei.
Kabla ya kuwasili mjini Morogoro mwishoni mwa juma lililopita, Simba walikuwa wameweka kambi mkoni Iringa, baada ya ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Njombe Mji.
Kwa wenyeji wa mchezo wa hii leo Mtibwa Sugar ambao wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 30, wamepania kuvuruga rekodi ya Simba ya kutopoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi, kwa kuhakikisha kunaifunga kwa mara ya kwanza na kuondoka na alama tatu muhimu.
Kinachoongeza utamu katika mpambano huo ni kiwango bora cha Mtibwa Sugar kwa siku za karibuni wakiwa imetoka kuwafunga vigogo wawili mfululizo ikianza na Azam FC katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports na kisha kuifunga Singida United mabao mabao matatu kwa sifuri katika mchezo wa ligi.
Chanzo: Dar 24

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here