Mourinho: Daima Nitamheshimu Wenger. Anastahili Heshima Kubwa.

0
1
Boss wa Manchester United  Jose Mourinho amesema daima amekuwa mwenye heshima kubwa sana kwa Boss mwenzie wa Arsenal The Gunners Mzee Arsene Wenger pamoja na kuwepo kwa Ugomvi usioisha baina yake na Kocha Arsene Wenger ambaye anatarajiwa kuondoka na kuacha kuwa Mwalimu wa Washika Bunduki hao.
Mourinho and Wenger
Wenger ametangaza siku ya Ijumaa- leo Tar.20/04/2018 kwamba atang’atuka na kustaafu kuwa Kocha wa timu ya Arsenal baada ya kuiongoza timu hiyo kwa jumla ya miaka 22
“ Kama yeye ana furaha basin a mimi nitakuwa mwenye furaha, kama anaondoka akiwa mwenye majonzi basi namimi sitakuwa mwenye furaha kabisa”! Mourinho alimwambia Mwandishi wetu wa SPOTI.TZ.  Ameendelea kusema: “Daima nimekuwa nikiwatakiwa wapinzani wangu.kila lililo jema”
“Bwana Wenger na Arsenal kwa miaka mingi sana Wamekuwa wapinzani wakubwa wa Sir Alex Ferguson, hivyo nina uhakika kwamba sisi kama Timu tutampa Wenger heshima anayostahili” Mourinho ameongeza.

“Ninamtakia mafanikio mema, ila ninachoomba ni kwamba asistaafu kufundisha mpira, ni mtu muhimu katika ulimwengu wa soka. Hivyo nina tarajia sana hatastaafu”. Aliongeza Mourinho

Na: Sabby@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here