Mourinho Amtetea Paul Pogba

0
4

Jose Mourinho ameamua kumtetea mchezaji wake Paul Pogba baada ya ‘Super Star’ huyo kutajwa kuwa Asiye na heshima na mchezaji wa zamani wa United Pau Scholes.
Mchezaji huyo wa zamani wa United, Scholes alimlaani Pogba kwa mchezo wake wa kiwango cha chini kabisa na kisicho na heshima kwa kocha wake siku ya Juma pili , United walipopokea kichapo kilichowaacha na mshtuko kutoka kwa timu ya West Bromwich Albion.
Maoni ya Scholes yaklikuja wakati ambao kuna taarifa zinazoendelea chini kwa chini kwamba Mourinho yupo tayari na ana mpango wa kumuuza Pogba kutokana na kiwango kisichoridhisha ambacho amekuwa akikionesha Pogba kwa misimu miwili mfululizo.
Lakini itakumbukwa kwamba ni Pogba huyuhuyu alionesha kiwango cha juu katika mchezo United walioucheza dhidi ya Bournemouth siku ya juma tano wiki iliyopita na kuibuka na ushindi wa 2- 0 baada ya kumuwekea Lukaku mpira mzuri na kufunga goli la pili.
Alipoulizwa na Spoti Tz kuzungumzia maoni ya Scholes juu ya Pogba, Mourinho alisema “Sikubaliani na maoni Scholes, ila ninakubali kwamba haukuwa mchezo mzuri kwetu dihidi ya West Brom. Kwa hilo nakubali”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here