Mohamed Salah: Ninataka kushinda Kiatu Cha Dhahabu EPL

0
5
Mohamed Salah

Mshambuliaji hatari wa timu ya Liverpool, Mohamed Salah anatarajia kuendelea kubaki kileleni mwa orodha ya wafungaji magoli katika ligi ya Uingereza na kushinda Kiatu cha dhahabu katika msimu huu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri ameongeza kwamba wachezaji wenzie wa Liverpool wameapa kumsaidia ili kufikia malengo yake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ameshafunga jumla ya magoli 30 katika michezo yake 32 aliyoichezea Liverpool katika Ligi ya Uingereza.
Salah ana magoli 4 zaidi ya Harry Kane anayemfuatia katika orodha ya wafungaji EPL.Salah bado ana michezo 4 mkononi ili kumaliza Ligi hiyo.
“Wachezaji wenzangu wanajaribu sana kunisaidia ili kufunga magoli kwasababu wanajua nipo katika nafasi nzuri ya kushinda kiatu cha dhahabu. Mwisho wa siku inakuwa ni jambo la mchezaji binafsi lakini pia inasaidia timu kupata alama na heshima” Salah aliliambia Spoti Tz.
“Namna tunavyocheza ni vizuri sana, na unaweza kuona Mashabiki wanafuraha sana msimu huu, na inanipa faraja na furaha kubwa. Najisikia kama wanataka mimi nishinde kitu Fulani”
“Ni michezo minne ya mwisho, kwahiyo ni wazi kwamba ninacheza kwaajili ya mafanikio hayo”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here