Mkude kuikosa Lipuli Jumamosi

0
6
KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude, ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Lipuli FC utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora, Iringa kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Mkude, kiungo aliyepandishwa kutoka katika kikosi cha timu ya vijana ya umri chini ya miaka 20 (Simba B), juzi katika mechi dhidi ya Tanzania Prisons alipata kadi ya tatu ya njano na hivyo hatastahili kucheza mechi hiyo inayofuata.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Haji Manara, alisema kuwa kikosi cha timu hiyo kinatarajia kuanza safari ya kwenda Iringa leo kikiwa na wachezaji wake wote.
“Mechi ni Jumamosi, tumepokea barua kutoka bodi ikieleza mabadiliko hayo, timu itasafiri Jumatano alfajiri kuelekea Iringa…baada ya mechi itareje na tutawapa ratiba kuelekea mchezo wetu na Yanga,” alisema Manara.
Chanzo: IPP Media

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here