Maxime: Tutapambana hadi dakika ya mwisho

0
7
 Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, alisema bado anahitaji kupambana ili timu yake iweze kujinusuru na panga la kuteremka daraja.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, alisema bado anahitaji kupambana ili timu yake iweze kujinusuru na panga la kuteremka daraja.
Maxime alisema msimu huu umekuwa “mbaya” kwa Kagera Sugar kwa sababu wachezaji wake wamekuwa wakipambana kucheza soka la kiwango cha juu, lakini wanakosa bahati ya kupata ushindi.
“Ukisikia msimu mbaya, gundu au fungu la kukosa, basi ndio vitu vinavyotuzunguka, ila hatujakata tamaa, tutapambana mpaka dakika ya mwisho ya msimu, tunaamini nafasi ya kubaki Ligi Kuu tunayo,” alisema kocha huyo na nahodha wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars).
Aliongeza kuwa ushindani wa mbio za ubingwa na zile za kushuka daraja zimeifanya ligi kuwa na ushindani zaidi msimu huu kwa sababu timu zinapishana pointi chache katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha klabu 16 kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Simba ya jijini Dar es Salaam inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, ndio vinara wa ligi hiyo inayotarajiwa kumalizika Mei 26, mwaka huu na kutoa timu itakayoiwakilisha Tanzania Bara katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Majimaji ya Songea, Ruvuma yenyewe inaburuza mkia katika msimamo huo.
Chanzo: Ipp Media

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here