MASUMBWI: Manny Pacquiao Kurudi Ulingoni Julai 15. Soma habari yake.

0
1

Manny Pacquiao

Manny Pacquiao, ambaye ni mwana masumbwi na mwanasiasa kwa Kifilipino, yupo mbioni kurudi ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya takribani mwaka mmoja toka alivyopigana ulingoni.
Bingwa huyo mara nane wa Dunia atapambana na Lucas Matthysse, bondia wa Argentina anaeshikilia mkanda wa World Boxing Association (WBA) welterweight. Pambano lao linatarajiwa kufanyika mwezi Julai 15, Nchini Malaysia katika mji wa Kuala Lumpur.
Wakati akitangaza kurudi  kwake huko katika ulimwengu wa Maswumbwi katika mkutano alioufanya na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila, Pacquiao alisema: 
“ Muda wangu wa kupambana haujaisha bado na ndiyo maana ninajitahidi sana na nitapambana sana kwaajili ya pambano hili la Julai 15.”
“Sina utabiri wa kuwapeni, lakini ninawaambieni nitafanya kila linalowezekana ili kushinda “ aliongeza bondia huyo mwenye umri wa miaka 39. 

Manny Pacquiao aliandika katika ukurasa wake wa Twita akisema:

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here