Makahaba Waahidi Huduma Bure kwa Timu ya Taifa wakifuzu AFCON

0
16
Chama cha Makahaba Nchini Nigeria “Association of Nigerian Prostitutes” (ANP) Kimeisifia Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Nigeria, The Super Eagles, kwa kuendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yanayowakabili.
Chama hicho sasa kimekuja na ahadi kemkemi kwa wachezaji wa Timu ya Nigeria, ikiwa Nigeria watafanya vizuri katika mechi zote za awali za AFCON. Chama hicho kimetangaza kwamba: kama wanawake wazalendo wa Nchi yao, ambao wanaitakia mema na mafanikio timu yao na Taifa kwa Ujumla, wanaahidi kutoa zawadi ya huduma ya ngono bure kwa wachezaji hao. Wanaamini wao wana vivutio vyenye thamani mbele ya wachezaji hao na hivyo kuwapa morali zaidi ya ushindi.

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu mkuu wa chama hicho, bibi Jessica Elvis, ameitaka timu ya Taifa kuhakikisha safari hii wanarudi na kombe na hivyo kulifanya Taifa la Nigeria “proud”

“Tunataka kuwaambia wazi kwamba wanayo sapoti yetu, tunawapa ahadi kwamba wote hapa tunafanya kila liwezekanalo kwa ajili ya Taifa letu, hivyo wao wafanye kazi kwa nafasi yao na sisi pia tunawaahidi kufanya kazi kwa nafasi yetu kwa kadri itakavyowapendeza ili kusonga mbele zaidi” alisema bibi Jessica Elvis.
Alisistiza kwamba wana ukaribu wa hali ya juu sana na usio na mashaka na Super Eagles, hivyo wanafanya kila juhudi kuwa sehemu ya mafanikio ya Timu hiyo! 

Ameongeza kwamba: “Kama Super Eagles watarejea nyumbani na Kikombe basi Tutatangaza wiki ya huduma bure kwa Super Eagles tu!” hii ikiwa na maana kwamba hakutakuwa na huduma hiyo Nchini Nigeria kwa wasiokuwa wachezaji kwa muda wa wiki nzima! Poleni ndugu wateja huduma itasitishwa kwa kazi maalumu! Maajabu ya Nigeria hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here