Madrid Wampa Ronaldo Mshahara Wa Kufuru! Mshahara wake Mpya ni Maajabu !!

0
14

Superstar wa Kireno Cristiano Ronaldo CR7, anatarajiwa kupewa mkataba mpya wenye Maslahi na Malipo makubwa na Timu yake ya Real Mdrid. Kabla ya kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia.
CR7
Mreno huyo aliyepachikwa jina la Mashine ya Kutengeneza magoli,amekuwa kwa kiasi kikubwa akihusishwa na kuihama Timu yake ya Madrid kwa kipindi cha miezi ya hivi karibuni. Inaarifiwa kwamba 
Ronaldo aliwaambia mabosi wa Madrid kwamba angeondoka katika msimu wa joto uliopita baada ya mgongano na kutokukubaliana kati yake na Klabu juu ya masuala ya ongezeko la malipo yake.
Ronaldo alikuwa anataka kuwa analipwa sawasawa  au zaidi ya kiasi anacholipwa Mchezaji wa Kibrazili anaeichezea PSG ya Ufaransa Neymar JR ambaye alihamia PSG kwa  kuvunja rekodi ya usajili Duniani, aliposajiliwa kwa kitita cha Euro 200m.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Madrid zilizolifikia SPOTI.TZ  zinasema kwamba Madrid hatimaye wanaelekea kukubaliana na madai ya Ronaldo. Hii huenda ni kutokana na mchango na juhudi alizozionesha Ronaldo katika Mashindano ya La Liga na yale ya UEFA.
Miongoni mwa Mabosi wa Madrid, Jose Angel Sanchez, amemwambia Ronaldo kwamba Timu ina mpango wa kuongeza kiasi kikubwa cha pesa kama mshahara wake kutokana na jitihada ambazo Ronaldo amekuwa akizionesha.
Inakadiriwa kwamba Ronaldo katika dili hili jipya atatia kibindoni kiasi cha Euro 30m sawa na Paundi 26.3m kwa mwaka. Hili litakuwa ongezeko katika mshahara wake wa sasa ambao ni Euro 21m sawa na Paundi 18.4m
Ronaldo bado ana mkataba na Madrid hati 2021

Na: sabby@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here