Lwandamina huyu hapa jukwaani na mvinyo akishuhudia zesco inashinda ugenini

0
2Kocha George Lwandamina ameishuhudia klabu ya Zesco United kwa mara ya kwanza ikiwa kibaruani jana dhidi ya Lusaka Dynamos katika mchezo wa ligi kuu nchini humo.

Lwandamina ameshuhudia mchezo huo kwa mara ya kwanza ikiwa ni siku kadhaa akiwa ameondoka nchini kuitumikia klabu ya Yanga.

Kocha huyo ameutazama mchezo wa jana akiwa jukwaani huku timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini.

Lwandamina alionekana akitazama mechi hiyo huku akipata mvinyo wake wakati mchezo unaendelea dhidi ya Lusaka Dynamos.

Tayari Lwandamina ameshachukua tena kitu cha Ukocha Mkuu ndani ya Zesco United kufuatia kutangazwa rasmi na uongozi wa timu hiyo juzi Jumatatu.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here