LIVERPOOL YAIPIGA MAN CITY 2-1 ETIHAD NA KUTINGA NUSU FAINALI

0
4

Roberto Firmino na Mohamed Salah wakishangilia baada ya kuifungia mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Manchester City kwenye mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne. Salah alifunga la kwanza dakika ya 56 na Firmino la pili dakika ya 77, kufuatia Gabriel Jesus kuanza kuifungia Man City dakika ya pili Uwanja wa Etihad na sasa Liverpool inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-1 baada ya kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Anfield wiki iliyopita

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here