Koffi Olomide Aalikwa Tena Kenya

0
3

Mwanamuziki wa Dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Koffi Olomide anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha nchini Kenya hivi karibuni ikiwa ni mara ya kwanza tangu afukuzwe nchini humo mwaka 2016.

Mnamo July 2016, Olomide alikamatwa na polisi wa Kenya na kurudishwa nchini DRC baada ya kusambaa kwa video iliyoonesha mwanamuziki huyo akimpiga mchezaji wa bendi yake wa kike kipindi akiwa jukwaani.

Jana April 13, 2018 alitangaza kualikwa nchini Kenya kufanya show kwenye mkutano mkubwa wa viongozi 47 wa majimbo ya nchi hiyo utakaofanyika Kakamega.
Chanzo: Udakuspecially

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here