Kocha mpya bayern ataeanza kazi july 2018

0
4Uongozi wa Bayern Munich umetangaza kuingia mkataba wa miaka mitatu na KochaEintracht Frankfurt, Niko Kovac.

Kovac atakuwa anachukua mikoba ya Jupp Heynckes ambaye alikuwa akiitumikia klabu hiyo kwa muda kufuatia kuondoshwa kwa Carlo Acelotti aliwezesha Bayern kuchukua taji la 6 mfululizo katika ligi.


Heynckes anajiandaa kuondoka Bayern Munich huku akiwa anajiandaa kukabiliana na Real Madrid katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid, Aprili 24 2018.

Kocha huyo (72) aliyewahi kuwa Nahodha wa timu ya taifa ya Croatia, aliichezea Bayern mwaka 2001 mpaka 2003.

Kovac ataanza rasmi kuitumikia Bayern Munich Julai mwaka huu wa 2018.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here