Kamusoko atajwa Simba SC

0
3

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, juzi alihudhuria mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Singida United.

Mfaransa huyo alikuwa jukwaani kuwasoma watani zake kuelekea mechi dhidi yao Aprili 29 2018 iyakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lechantre alionekana akiwa na Notebook huku akiandika vitu kadhaa wakati akitazama mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Lechantre alimuulizia kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko akitaka kujua wapi alipo baada ya kushindwa kumuona kikosini.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, limeeleza kuwa Lechantre alisema hajamuona Kamusoko Uwanjani na hajui tatizo ni nini, kisha akasema kukosekana kwake na baadhi ya wachezaji kunaifanya Yanga isipate matokeo mazuri.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here