Kaka amtaja Mourinho kama ni muuaji wa soka lake.

0
3

Mwaka 2007/2008 Ricardo Kaka alikuwa katika kiwango cha juu sana kisoka, hii iliwashawishi Real Madrid kuzama mfukoni na kutoa £56m ambayo iliwashawishi Ac Milan kukubali kumuuza Kaka.

Lakini alipofika Real Madrid maisha yalibalika sana, ukiacha majeraha yaliyokuwa yakimsumbua lakini Kaka kiwango chale kilionekana kushuka sana, na Kaka huyu akawa sio yule wa Milan.

Kaka akaanza kuanguka technically na physically na hii ni akiwa chini ya kocha Jose Mourinho, baada ya safari ndefu ya vikwazo hatimaye mwaka jana Kaka aliamua kutundika daluga.

Lakini Kaka amefunguka moja ya sababu kubwa za yeye kuboronga Real Madrid, ni Jose Mourinho. Kaka amekiri kwamba chini ya kocha huyo hali ilikuwa ngumu sana kwa na alishindwa kuendana naye kabisa.

“Mwaka 2009 nillikubali kujiunga na REAL MADRID lakini nilipotea kabisa, kwani JOSE MOURINHO alikuwa kocha mgumu sana kwangu. ila tulikuwa tunaheshimiana lakini uhusiano wetu ulichanganya sanaa”.

Kaka anasema kuna wakati aliamini atapewa na Mourinho, lakini kocha huyo hakumpa nafasi ya kuonesha nini alichonacho na hii ikawa inazidi kumpoteza katika soka.

Pamoja na yote hayo lakini Kaka hakujali aliendelea kuamini atapewa nafasi, aliendelea kufanya mazoezi na kumuomba mungu apewe nafasi lakini mwisho wa siku akagundua hawezi kufanya kazi na Mourinho.

Pamoja na yote lakini Kaka anadai Mou alimtumia message kuwa yeye ni mchezaji mpambanaji japo wakati huo tayari Mou alishakwenda Chelsea, na Kaka msimu huo huo alirudi Milan.

Posted by Lebab
source: Espn

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here