Harry Kane anaamini atamshinda Mohamed Salah kwa ufungaji wa mabao.

0
4

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane amesema anaamini atamshinda nyota wa Liverpool Mohamed Salah na kutwaa tuzo ya mfungaji mabao bora Ligi ya Premia msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa England amefunga mabao 24 msimu huu.
Hata hivyo, ameachwa nyuma na Salah ambaye ni raia wa Misri kwa mabao matano.

Kane, 24, anapigania kuwa mchezaji wa kwanza tangu Thierry Henry kuongoza kwa ufungaji wa mabao Ligi Kuu ya England kwa misimu mitatu mtawalia.

“Naamini ninaweza kufanya hivyo. Bado kuna mechi zilizosalia kuchezwa,” Kane amesema.

“Lazima niendelee kuangazia uchezaji wangu. Siwezi kudhibiti anachofanya yeye

“Bila shaka kama mshambuliaji, itakuwa vyema sana kuishinda buti ya dhahabu tena na nitaendelea kutia bidhii kuanzia sasa hdi mwisho wa msimu.”

Kane ambaye amekuwa akiuguza jeraha la kifundo cha mfuu amerejea kucheza baada ya kupona.

Mshindani wake Salaha, 25, hata hivyo hakucheza debi ya Merseyside Jumamosi kutokana na jeraha la mtoki alilopata akichea Liverpool mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano ambapo waliwalaza Manchester City mechi ya mkondo wa kwanza robo ainali.

Kane ana nafuu kidogo ukizingatia kwamba Spurs wamesalia na mechi sita za kucheza Ligi Kuu lakini Liverpool wana mechi tano pekee.

Na huenda bado akafaidika zaidi katika kupunguza mwanya kati yake na Salah iwapo atahesabiwa bao la ushindi dhidi ya Stoke Jumamosi, ingawa kituo cha wasimamizi wa mechi cha Ligi ya Premia siku hiyo kiliamua kwamba Christian Eriksen ndiye aliyefunga bao hilo.

Spurs walilaza Stoke 2-1. Mabao yote mawili yalihesabiwa kuwa ya Eriksen.

Kane anasisitiza kwamba mpira frikiki iliyopigwa na Eriksen ulimgusa begani kabla ya kumbwaga kipa wa Stoke Jack Butland na kuingia wavuni.

Spurs wamepanga kukata rufaa uamuzi huo wa kumpa kiungo huo wa kati kutoka Denmark bao hilo na badala yake wanataka lihesabiwe kuwa la Kane “Naapa kwa uhai wa binti wangu kwamba niliuguza mpira huo, lakini hakuna jambo jingine ninaloweza kulifanya,” Kane amesema.

“Wakiamua kubadilisha, watabadilisha. Wakiamua kuamini msimamo wangu, watakuwa wameusikia msimamo wangu.
“Mambo ni vile yalivyo – muhimu zaidi ni kwamba tulishinda mechi”.

WAFUNGAJI 10 MABAO EPL MPAKA SASA HIVI..
Mohamed Salah, Liverpool 29
Harry Kane, Tottenham 24
Sergio Agüero, Man City 21
Raheem Sterling, Man City 16
Jamie Vardy, Leicester 16
Romelu Lukaku, Man Utd 15
Roberto Firmino, Liverpool 14
Son Heung-min, Tottenham 12
Álvaro Morata, Chelsea 11
Eden Hazard, Chelsea 11

Posted by Lebabtv
Source: The Guardian

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here