Guardiola: Man City Tunatafuta Heshima, Lazima tushinde Mechi zote Tano

0
7

Pep Guardiola amesisitiza kwamba hata kama wameshatwaa ubingwa wa EPL, inawapasa sasa wacheze kwa lengo la kuweka historian a heshima katika Ligi Ya Uiengereza, hivyo lazima kushinda katika Mechi zao zote tano zilizosalia.
Pep Guardiola (Meneja wa Manchester City)
City watakuwa nyumbani Jumapili ya Kesho baada ya Guardiola kushinda taji hilo la kwanza akiwa katika Ligi Ya Uingereza baada ya Kuwafunga Tottenhem na Mshindani wake wa karibu Manchester kufungwa na West Bromwich.
Guardiola ameshinda taji hilo la EPL  baada ya kufanya hivyo akiwa Katika Ligi ya La Liga na Barcelona kabla hajatua Ujerumani akiwa na Bayern Munich ambako nako alishinda taji lake.
Boss huyo wa City, anasema kwamba anajua wachezaji wake wanaweza kupunguza kiwango na kasi yao ya uchezaji kwasababu tayari wana kikombe mkononi, sasa anadhani kwamba Timu ikiwa na lengo la kutafuta heshima na kuweka historia, basi lazima wacheze kwa jitihada zote.
“Lengo langu ni kuifukuzia Historia ya Chelsea katika EPL ambapo Chelsea waliweka Historia ya kushinda kombe wakiwa na alama 95 katika msimu wa 2004/05” Amesema Guardiola.
 City kwa sasa wana alama 87 na michezo mitano mkononi huku wakiwa tayari wametawazwa mabingwa wa EPL.

Na sabby@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here