Diamond, Nandy kupanda kortini

0
9
SERIKALI imesema inaangalia namna ya kuwafikisha mahakamani wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, akiwamo, Naseeb Abdul “Diamond Platnumz” na Faustina Charles “Nandy” kwa makosa ya kusambaza picha za video zisizo na maadili mitandaoni, imeelezwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ulanga(CCM), Goodluck Mlinga.
“Tunayo sheria lakini ilikosa kanuni za kubana maudhui hasa upande wa mitandao, kwa sasa tumeshatunga kanuni na zimeanza kufanya kazi.
“Kuna baadhi ya wasanii walianza kufanya uhuni kwenye mitandao jana,  tumeweza kumkamata mwanamuziki nyota Diamond , amefikishwa polisi na anahojiwa kufuatia picha alizorusha,” alisema.
Alisema pia ameagiza Nandy naye apelekwe polisi na  kuhojiwa na vile vile wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani huku pia akitoa wito kwa vijana kutoifanya mitandao ya jamii kuwa “kokoro” la kupeleka kila kitu na kuwakumbusha kwamba tamaduni lazima zilindwe.
IPP Media

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here