Diamond amfagilia Vanessa Mdee, “Unapambana sana Vee”

0
4

Msanii
Diamond Platnumz amemfagilia mrembo Vanessa Mdee kutokana na jitihada
zake anazofanya kila kukicha za kuupambania muziki wake uzidi kufika
mbali zaidi.
Mkali
huyo wa WCB kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika ujumbe huo wa
kumsifia Vee Money huku akimtakia baraka tele kwenye safari yake hiyo.
“Unapambana Sana Vee.. Mwenyez Mungu azidi kukufungulia Kwenye kila la Kheri Uliombalo @vanessamdee ??,” ameandika Diamond.
Diamond
amewahi kufanya kazi na Vanessa kwa kumshirikisha kwenye ngoma yake
inayoitwa ‘Far Away’ ambayo inapatikana kwenye albamu yake ya A Boy From
Tandale.
Chanzo: Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here