''Man City inaweza kukosa ubingwa'' – Guardiola

0
2

Kuelekea mchezo wa leo wa ligi kuu ya England kati ya vinara Manchester United na Tottenham, kocha Pep Guardiola amesema timu yake bado ipo kwenye hatari ya kukosa ubingwa wa EPL msimu huu.

”Inawezekana kabisa tukakosa ubingwa ni vitu ambavyo vinatokea kwenye mchezo wa soka, hakuna aliyeamini kama tunaweza kupoteza mchezo hata wachambuzi walisema Man City haiwezi kupoteza alama lakini leo tuko hapa bado tunatafuta ubingwa”, amesema.

Aidha Guardiola ameongeza kuwa kwasasa timu yenye nafasi kubwa ya kufanya vizuri ni Manchester United ambayo amedai kwasasa ipo kwenye wakati mzuri tangu msimu uanze hivyo wana nguvu kubwa ya kufanya vizuri.

Man City leo itakuwa ugenini kucheza na Tottenham Hotspar huku ikiwa kilelenni kwa tofauti ya alama 13 na Man United inayoshika nafasi ya pili hivyo kama Man City leo atapata ushindi atakuwa amejihakikishia ubingwa. 
Chanzo: Udakuspecially

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here