Buffon amfananisha mwamuzi na muuaji

0
2Kipa mkongwe nchini Italia, Gianluigi Buffon ameamsha mashambulizi dhidi ya mwamuzi Michael Oliver kwa kumuita muuaji.

Kama haitoshi, Buffon amesema mwamuzi huyo hana moyo katika kifua chake.

Mara baada ya Juventus kurejea kwa Italia, Buffon amesema Oliver kutoka Uingereza ameipendelea waziwazi Real Madrid kwa kuipa mkwaju wa penalti ambao hawakustahili.

Juventus iliitwanga Madrid kwa mabao 3-1 kwao Santiago Bernabeu lakini ikang’oka katika hatua hiyo ya robo fainali kutokana na bao la mkwaju wa penalti waliopata Madrid katika dakika za nyongeza.

Mwamuzi alipuliza filimbi kuashiria faulo baada ya Lucas Vazquez kuamgushwa katika dakika ya 90+3.

Baada ya maneno makali, Buffon alitolewa nje kwa kadi nyekundu jambo ambalo lilizidisha hasira za mashabiki wa Juventus na wale wasioiunga mkono Madrid.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here