Barcelona: "Maumivu ya Kutolewa UEFA bado yanatutesa" Kocha anena…

0
7
Ernesto Velvede

Kocha wa Barcelona Ernesto Valvede amesema kwamba Timu yake na yeye mwenyewe kama mwalimu walipata fundisho la Karne kutokana na kichapo kilichowaletea mshituko katika Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya. Somo walilolipata ni kwamba Wasijaribu hata siku moja kujiona wao ni bora sana na kuchukulia baadhi ya michezo kiurahisirahisi kama vile wao ndiyo wamiliki wa Ushindi daima.
Velvede ametoa hayo ya moyoni wakati ambao timu yake inajiandaa kukutana na Sevilla katika fainali ya Kombe la Mfalme nchini Uhispania.
Kocha huyo ana nafasi ya kushinda kombe hilo la kwanza kwake akiwa kama Kocha wa Barca. Barca wanao uwezekano wa kushinda kombe la La Liga pia, uwezekano wa kunyakua makombe mengi zaidi ulitibuliwa na Kichapo cha 3-0 kutoka AS Roma katika mashindano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya na kuwatoa nje ya Michuano hiyo.
Sabby@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here