Barcelona Wajihakikishia Ubingwa wa La Liga 2017/18. Wana mchezo mmoja tu Kulinyakua Kombe.

0
2
Barcelona inasubiria  ushindi mmoja pekee kujipatia taji la 25 la ligi ya La Liga baada ya Atletico Madrid kupoteza kwa Real Sociedad.
Barcelona sasa itashinda taji la La Liga iwapo itashinda mechi yake dhidi ya Deportivo Lacuruna tarehe 29 Aprili.
Barca ilimaliza ya pili msimu uliopita wakiwa pointi tatu nyuma ya mabingwa watetezi Real Madrid. 
Uwezekano mkubwa wa Barca kunyakua kikombe hicho cha La Liga msimu huu unatokana na Atletico Madrid kufungwa 3-0 na Real Sociedad
Kikosi hicho cha Diego Simeone hakikuonyesha mchezo mzuri na kikajikuata nyuma wakati Willian Jose alipomalizia pasi iliopigwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United Adnan Januzaj.
Mchezaji wa ziada Juanmi alifunga bao la pili katika dakika za lala salama kabla ya kuongeza bao lake la pili katika dakika ya mwisho kabisa na kuwaacha Atletico hawana cha kufanya.
Atletico ndiyo timu iliyokuwa inaipa Barca changamoto kiasi katika mbio zake za kuwania ubingwa huo.  Kwa sasa Atletico  wako pointi 12 nyuma ya Barcelona na  wanakutana na Arsenal katika awamu ya kwanza ya mechi ya nusu fainali ya kombe la Europa  tarehe 26 Aprili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here