AZAM WAIOMBA TFF KUWASOGEZEA MBELE MECHI YAO DHIDI YA NJOMBE MJI

0
2

UONGOZI wa Azam FC umeomba mchezo wao dhidi ya Njombe Mji usogezwa mbele kutokana na muda mchache waliopumzika baada ya kumalizana na Ruvu Shoting ya Mlandizi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa Azam Jaffary Maganga amesema wameomba mchezo kusogezwa mbele ili kupata nafasi ya kujiandaa ikiwa ni jana wametoka ugenini kucheza na timu ya Ruvu shooting.

“Tumeandika barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania( TFF) kuomba mchezo dhidi ya Njombe Mji ya mkoani Njombe usogezwe mbele badala ya kuchezwa kesho ikiwa sheria za FIFA zinasema inatakiwa kupumzika saa 72 na si 48,”amesema.

Mchezo huo uliotarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la Azam Complex Chamazi.Ambapo kikosi hicho cha Azam kimerejea jana hiyo hiyo kutoka Mlandizi kuendelea kujifua na mazaoezi kukabilia na Njombe Mji katika mchezo wao ujao.

“Tumerejea jana usiku kutoka Uwanja wa Mabatini Mlandizi tulipomaliza tu mechi na kikosi kipo mazoezini kujiandaa nadhani nnajua Njombe Mji ni timu nzuri pia”amesema Jaffary Maganga.

Azam FC walikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ruvu Shoting na kuendelea kubaki nasafi ya 3 wakiwa na alama 45,huku vinara Simba wakiendelea kujikita Kileleni kwa alama 52 na Mabingwa watetezi Yanga wao wakishikilia nafasi ya pili kwa pointi 47,katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Chanzo: Issa Michuzi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here