Atletico vs Arsenal 1-1, Mashabiki wachekelea wasema lazima mspain atoke.

0
4
Lacazette akiifungia Arsenal bao la pekee 
Antoine Griezmann aliiadhibu safu ya
ulinzi ya Arsenal katika dakika za lala salama huku timu ya Atletico
iliokuwa na wachezaji 10 kupata sare katika nusu fainali ya kombe la
bara Yuropa iliofanyika katika uwanja wa Emirates.

Wageni hao wa
Uhispania walilazimika kurudi nyuma na kulinda lango lao katika kipindi
kirefu cha mchezo baada ya beki Sime Vrsajko kupewa kadi nyekundu kwa
kucheza visivyo katika dakika 10 za kwanza.
Huku kocha wao pia naye akiondolewa katika eneo la
kocha na kulazimishwa kuketi na mashabiki baada ya kumkaripia refa kwa
hatua yake.
Uhispania ilinusurika mashambulizi makali kutoka kwa
mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette akigonga mwamba wa goli
katika fursa ya wazi ya Arsenal.
Griezmann akifunga bao lililoipatia Atletico nguvu mpya katika awamu ya pili ya mechi za Yuropa

Lacazette alifunga krosi ya Jack Wilshere baada ya saa moja na kuipatia Arsenal fursa ya kufuzu katika fainali ya kombe hilo .
Lakini
ikiwa zimesalia dakika nane pekee, Griezman alivamia lango la Arsenal
baada ya beki Laurent Kolscieny kufanya masikhara na kuwapatia Atltico
Madrid fursa ya kufuzu nyumbani siku ya Alhamisi ijayo.
Mashabiki wa Arsenal waliwachwa wakilalama kuhusu
timu hiyo kushindwa kukamilisha fursa za wazi katika mechi ya mwisho ya
nyumbani ya yuropa ya Arsene Wenger.
Arsenal sasa italazimika
kuvunja safu ya ulinzi ya Atletico ambayo imefungwa mara nne pekee
katika ligi ya La Liga msimu huu ili kuweza kuwa na matumaini ya
kuongeza ufanisi wa Wenger katika uongozi wake wa miaka 22 wakati
watakapofuzu kwa fainali Mei 16.
Chanzo-BBC swahili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here