Ajibu, Dante wazidi kuipa presha Simba

0
4


Wachezaji wa Yanga waliokuwa majeruhi wanazidi kuimarika mazoezini kambini mjini Morogoro baada ya kurejea siku kadhaa zilizopita.

Wachezaji hao ambao ni Ibrahim Ajibu na Andrew Vincent walianza mazoezi siku moja baada ya Yanga kuweka kambi Morogoro ambapo taarifa zinaelezwa hali yao inaendelea vizuri.

Kuendelea kuimarika kwa wachezaji hao kunaipa nafasi Yanga kutengeneza silaha zao vizuri kuelekea pambano lao dhidi ya Simba.

Mbali na hao, Amis Tambwe pamoja na Donald Ngoma nao wameshajiunga na wachezaji wenzao kambini wakiendelea kujiandaa na mechi hiyo yenye hisia kali kwa mashabiki.

Mechi hiyo itapigwa Jumapili ya wiki hii Aprili 29 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here