Aiseeh, CAF yaifanyia umafia yanga

0
8Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limejichanganya kumzuia beki wao Kelvin Yondan kwa madai ya kuwa ana kadi mbili za njano.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kwa mujibu wa rekodi zao zinaonesha kuwa Yondani hana kadi mbili na badala yake Pato Ngonyani ndiyo alipata hizo kadi.

Ten ameeleza kuwa CAF wamekosea kufanya maamuzi hayo huku akidai Yondani ana kadi moja pekee na si mbili kama walivyosema.

CAF ilituma tarifa ya wachezaji wanne wa Yanga kuzuiwa kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC ya Ethiopia ambao walipewa kadi mbili za njano kila mmoja.

Wachezaji waliotajwa na CAF ni Papy Thsishimbi, Obrey Chirwa, Said Makapu na Kelvin Yondan.

Hata hivyo uongozi wa Yanga umesema utafanya mawasiliano na uongozi wa CAF ili kuona kama wanaweza wakalifanyia mabadiliko suala hilo.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here